Monday 23 November 2009

TANZANIA IMEJISAHAU

tanzania ni miongoni ya mataifa yenye utulivu utulivu huu usiwafanye watawala kufanya ndio misingi ya kukandamiza jamii fulani tumeshuhudia polisi wakitwa wazembe na waheshimiwa sipingi kwani hata walimu na wanajeshi nao utendaji kazi wao umeshushwa na upungufu wa maslahi duni na ukosefu wa vitendea kazi watawala wameamua kuwaingiza katika mtego utaowatofautisha na wananchi kwa kuwahusisha na ufisadi wa meremeta watawala wanatumia misingi ya nidhamu ya jeshi kutowajibika kujibu hoja yeyote iliyotolewa na mkubwa wako, napenda kusisitiza kwa watawala wasijaribu kutibua misingi mizuri ya jeshi na kulitwisha mzigo wa ufisadi, ningependa kuwafahamisha ya kuwa mzigo wa ufisadi ni vema wachague ni fisadi gani atayeubeba na si jeshi kwani utakua ni uonevu usiostahiri na utaoleta madhara makubwa kwa watawala wenyewe ni nani asiyefahamu kutoa kafara wapiganaji wetu kuna madhara gani? sipendi kuona watanzania tunapoteza misingi ya amani na utulivu ila nasita kuona ni wapi jahazi la tanzania linaelekea , vijana wapo tayari kulikomboa taifa lao kutoka katika dimbwi la umasikini hata kwa dhana duni ila watawala wawahakishie sera bora tunaweza kushiriki katika kilimo lakini taifa ni lazima litunze ardhi kwani sasa taifa linabinafsisha kwa wageni ningependa tusiliingize jeshi katika ufisadi ila ikibidi lishirikishwe kwenye uzalishaji na miradi kama nyumbu inaweza kuleta tija na heshima kwa jeshi letu sishangai kuona viongozi wakijisahau kwani ni kawaida kwa binadamu wasio na uwezo wa kukumbuka ni wapi walipotoka ni nani asiyejua ni askari wangapi wanalala njaa na kushindwa kusomesha watoto wao vyuo vikuu kutokana na sera za watawala wanaojari maslai yao na kutaka kujinufahisha kupitia wanyonge,natambua tanzania ni tajiri kwani mimi kama mwanachuo ninayesomea account and finance natambua nini kinaendelea, kikubwa kinachonisikitisha ni kitendo cha watawala kutaka kuliunganisha jeshi na wakoloni sijui wamelala na kusahau wanakata tawi waliokalia kwani ni nani atayemtoa mkoloni wanayempa ardhi yetu kutokana na ukuhadi wa viongozi wetu tazama watawala wanavyotumiwa kuteketeza maisha ya watanzania north mara (NYAMONGO) je inahitaji elimu ya chuo kutambua taifa lipo katika ukoloni mamboleo na ni upungufu wa afikiri unaosababisha umasikini wetu na kutumiwa kama mabwege na wakoloni na sasa mkoloni anasababisha kitendo cha kulipotezea imani jeshi letu ili iwe raisi kuja tena kwa kadri ninavyowafahamu watu wa kanda ya ziwa nachelea kusema serikari inaliingiza jeshi la polisi katika mgogoro usio na tija jeshi la polisi na wananchi nafahamu ya kuwa watawala wameamua kutumia jeshi vibaya kwa malengo ya kisiasa ili kuvunja sakata la ufisadi na kuendeleza ukuhadi wa wakoloni kama hawatambui ni kosa linaloweza kusababisha mabadiliko ya historia ya nchi na wao wasipate watu wa kuwatawala kwani ni nani mwenye furaha huko somalia..? kama si magaidi pekee najiuliza watawala wetu wanataka kuwa magaidi ..? wiishi kama somalia au wanapenda wawe kama MOBUTU SESESEKO....? ni kitu cha kushangaza kwa watawala wetu kutopenda kuwatumia wataalamu wetu sasa imefika wakati wanafikiri wanastahiri kujiheshimu wao tu na kutupia mzigo wa lawama kwa kila wanayemuona napenda kusisitiza ya kuwa wanajeshi si walimu kwani watawala wamewakandamiza kwa kipindi kirefu bila ya wao kujinasuo na kuongozwa na vibaraka wanaouza haki za walimu kwa SUZUKI NA RAV 4 , naipenda tanzania na nisingependa 2020 niwe mkimbizi katika ardhi ya wazungu kama wasomi wetu wwalivyozoea kudhani ya kuwa ulaya ndio kipimo cha mafanikio yao, najiuliza je watawala wanajaribu kuamsha mawe ili wao wanufaike au wawe wakibizi katika ardhi za wanaowafanya makuhadi wao na kutorosha rasilimali za taifa lao ,nisingependa kuelezea kwa undani zaidi kwani hata baba yangu aliwai kusema "WATAWALA NI JAMII YA WATU WASIO NA UCHUNGU NA RASILIMALI ZA NCHI ZAO NA NI WATU WASIOTESEKA NA VITA NA UMASIKINI WA TAIFA" nawatakia watanzania mafanikio na ushindi katika maisha ya kila siku na kushauri watawala wasiangamize kizazi kisicho na hatia MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU IBARIKI AFRIKA
GODWINI CHACHA
0718122081

No comments:

Post a Comment