Sunday, 22 November 2009

TANZANIA INAPOELEKEA

GODWIN CHACHA Says:
May 22, 2009 at 11:59 am

kama sisi wenyewe kwa wenyewe hatusaidiani je jini gani atasimamia haki na wajibu wa viongozi wetu? kama ilivyo kawaida yetu waTZ muda mwingi tunautumia kwa kulalamika badala ya kufanya kazi na kutetea haki zetu wananchi hawafahamu kuwa hospitali elimu ni haki ya msingi vikifuatiwa na barabara na maisha bora na watambue wana haki ya kuiwajibisha serikali kutokana na uzembe na ukosefu wa maendeleo na vifo visivyo vinavyotokana na afya duni je ni kesho au leo wataanza kuoji?au wanangoja watoto wetu waje kuoji?kama nikipata nafasi na fedha kama mafisadi nitatumia muda wangu kuwaelimisha kupitia gazeti langu sio kubaki na manung’uniko ya sisi waarabu tunaonewa .je wananchi wanaweza kutambua madini sio ya viongozi bali ni yao? je wananchi wanatambua njaa si haki yao? je kufa kwa mabomu mbagala si uzembe wao? je ajila si hisani?ukuhadi una mwisho? naogopa siku wananchi watapojua aya watadai walivyoibiwa? au watapigana na waliowaibia? kutokana na upeo wangu sitambui ni janga gani linakuja lanini nahisi tanzania inaelekea pabaya.je malaika gani wataiokoa kwani mapadri na masheha wanaelemewa.kama nikifika mwaka 2020 nitakuwa nimeshuhudia ninayofikiri. je baada ya mwakyembe kuwatetea wananchi atafuata nani? je zitto nae ataanza kama zamani? je slaa ataendelea na ushujaa? na je kikwete atakuwa raisi wa kwanza kutawala kipindi kimoja? nafikiri katika maswali yangu nahitaji miaka 10 kujiuliza maswali lakini tanzania pasipo na mabunge mawili ni bure.je baada ya sitta ni spika yupi? je sitta atakua raisi? kama ningeambiwa kuchagua kazi ningekuwa mwalimu kwani kuonewa nisingeogopa.yote haya najiuliza ni nani na lini tanzania iliuzwa? nani ameinunua? je hatatufukuza katika ardhi yake? je tutaenda wapi kama tukifukuzwa. enyi wazalengo badilisheni mfumo wa mapambano sifa binafsi haziwezi kulikomboa taifa maskini lenye rasilimali nyingi.je watanzania ni vivutio vya utalii na kama tukiendelea watalii hawata kuja kutuangalia?je nasi tujute kuzaliwa tanzania

MUNGU IBARIKI TANZANIA
GODWIN WA MZUMBE
0718122081

No comments:

Post a Comment