Tuesday 1 December 2009

NINI KIFANYIKE TANZANIA

NINI KIFANYIKE TANZANIA
Tanzania ni nchi iliyojengwa katika msingi wa ujamaa na kujitegemea, chini ya utawala wake, hayati baba wa taifa mwalimu julius k.nyerere.Ujamaa ni mfumo uliowapa fulsa sawa jamii yote ya tanzania upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii kama elimu afya nahata nafasi ya uongozi jamii yote bila ya kujali wametota katika jamii gani.Baba wa taifa aliweka misingi ya uongozi wazi, na hata tukawa na Azimio la Arusha, lililotamka wazi, nini kifanyike kwa viongozi na watu kwa ujumla.

Misingi hii ilisaidia kuwabana watu wenye uchu na ufujaji wa mali na rasilimali za taifa, kushindwa kufanya hivyo.Hatusemi kwamba chini ya utawala wa baba wa taifa hakukuwa na urasimu, kwani wote tunafahamu wakati mwingine, ugawaji wa bidhaa kama sukari na unga wakati mwangineulifanywa kwa urasimu(uranguzi) na watumishi wa serikali yake .
Lakini kikubwa tunachojivunia ni pindi tatizo lilipojitokeza hakusita kuchukua hatua, yeye kama kiongozi.
watu waliachishwa kazi na wengine ata kuchapwa viboko.

lakini misingiya taifa ilianza kubomoka katika utawala wa raisi Mwinyi,ambapo kulikuja kuibuka Azimio la Zanzibar.
Azimio la Zanzibar, Liliruhusu viongozi kuanza kujilimbikizia mali, na hata wachache kumilikishwa uchumi wa taifa, hapo ndipo pengo kubwa kati ya walionacho na wasionacho lilipoibuka.
Hatupingi jamii kutofautiana kwa kipato, lakini watofautiane kwa haki na si wengine kwa kuhujumu wenzao.

Ubinafsi ulianza kuota mizizi na pindi serikali ya hawamu ya tatu ya bwana Mkapa wakahitimisha ugawaji wa mali za umma kwa wachache.kukatokea na uhibukaji wa watu wenye uchu wa mali, sijui walitokea wapi. Kwani hata wengine ambao si watanzania wa kuzaliwa, waliona kuna fursa wakakimbia kuchukua uraia wa Tanzania, na kuanza kushiriki katika wizi wa mali za umma.

Cha kujivunia katika utawala wa tatu nchi haikutikisika na mshikamano bado haukuvuvinjika na wananchi hawakukata tamaa.
Katika awamu ya nne ikisadikika iliingia madarakani kwa michango mingi kutoka kwa watu binafsi.

Awamu ya nne Iliwapa wananchi tumaini ya kurejea kwa maisha bora, na upatikanaji wa huduma muhimu za jamii.Ilianza kwa kishindo na kila mtu akadhani ni wakati wa mabadiliko makubwa ya kiutawala na ya kuwa Taifa linaelekea ambapo,jamii yote itanufaika na rasilimali za Taifa lao.

OH sipende hata kuamini mambo yanayotokea katika Taifa letu,mbali na
kujilimbikizia mali , wachache wezi wamekuwa na sauti ya kuwatukana watu wanaotetea haki ya taifa lao.
viongozi wakuu wakitetea wizi uku utawala unaona.JE ndio sera za awamu hii?.Taifa linateteme na mbaya zaidi unasikia watumishi wakubwa katika uongozi wakisema wazi, kijana usihoji wizi, mbona siku yeyote taifa linaweza kuingia katika eneo ambalo historia ya amani katika nchi yetu ikatoweka.
Dini zimetengana,jamii imeanza kuzomeana kati ya wezi na wapinga wizi,Siasa imegeuka biashara,uporaji mkubwa wa rasilimali,uroo wa madaraka,
mgawanyiko wa matabaka, wazee na vijana, maskini na matajiri, udini,ukabila,kushindwa kuwa na falsafa yeyote inayojulikana ambayo taifa inaifuata,

Tunajiuliza nini mustakabali wa nchi,ninani atayeweza kurudisha mambo katika mstari?.
Si kugawanyika kwa viongozi bali tazama hata sekta ya habari, mafisadi wameanzisha vyombo vya habari. wakijitangaza na kujigamba hakuna mtu anayeweza kuwagusa,inamaana wao wananguvu kuliko serikali au wao ndio wamiliki wa serikali?,

Kwa upande wangu mimi ninaona suruhisho lipo katika njia mbili,
wananchi waitishe makongamano mbalimbali juu ya nini wanahitaj kifanyike, nini kusifanyike. Hatua gani wanahitaji zichukuliwe, au zisichukuliwe, na kama zisipochukuliwa ni nini cha kufanya?.

Pia misingi ya viongozi tunataka iweje? mfumo wa uongozi,kuanzia wa kisiasa mpaka kiutendeji,kwani madaraka ya raisi yawekwe wazi katika maamuzi, na uteuzina. Kama wakiona hakuna maamuzi ya msingi anayofanya nini kifanyike.je mbali na nguvu ya bunge kuisimamia serikali je wananchi wananafasi gani?.

Kwa upande wa pili ni kwa serikali kutangaza wazi kupitia, kwa raisi na watendaji wakuu ,nini msimamo wa serikali. Je nchi ihachwe iende kadri inavyotaka, au kuna mahamuzi magumu yanahitajika kuchukuliwa?. Uwajibikaji gani unahitajika. wapi kuna tatizo, wapi wanahitaji msaada?,nani wanasita kumchukulia hatua? kwanini wanasita kuchukua hatua?nini walikopa,kwa nani na wanahitajika kulipa nini?.

Mbali na misingi ya uongozi ni vipaombele gani vifuatwe kwani, kila bajeti tunasikia ina kipaombele chake,kama ni kilimo basi razima maamuzi yachukuliwe,ionekane wazi mikakati ya taifa, si mikakati ya kampeni.
Kama ni viwanda ni viwanda gani tunavitilia mkazo, mfano tunaweza kujitosa katika viwanda vya kilimo, na uboreshaji wa madini na vito vyetu.serikali na jamii inaweza kuendelea kwa namna hiyo.

Baba wa taifa aliwahi kutoa wazo la nchi kuendelea inahitaji, watu ardhi,siasa safi na uongozi bora,je tanzania ya sasa tunataka kupunguza vitu viwili, kutoka katika orodha yake? yani siasa safi na uongozi bora?.

Nahisi taifa ni wakati wake kujipima na kufanya marekemisho, hatua za msingi ili liweze kupata maendeleo, tunaipenda tanzania na daima hatupo tayari kuona inaelekea pabaya,tunaomba wananchi na viongozi kwa ujumla, kuchukua hatua, za kuboresha na kufanya marekebisha yanayoitajika. ili kuondoa manung"uniko,kuleta haki,huwajibikaji na kulinda rasilimali za taifa letu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
GODWIN CHACHA
0718122081
www.godwinchacha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment