Sunday, 22 November 2009

BODI YA MIKOPO NA UNYANG"ANYI

GODWIN CHACHA Says:
November 12, 2009 at 11:28 am

BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU INAPOGEUKA
KIKUNDI CHA WAHUNI NA WANYANG”ANYI
Ni miaka sasa imepita toka taifa lifikilie ni jinsi gani ya kuanzisha mfumo utaowawezeza watanzania wanaotakiwa kuendelea na masomo ya elimu ya juu kupata mikopo yakuwawezesha kujilipia karo na matumizi madogo ya kila siku kama chakula nk, kutokana na sheria ya uanzishwaji Taifa lilitoa ahadi mbali mbali kuwa hakuna mtanzania atayeshindwa kusoma kwa ajili ya kukosa mkopo,lakini kama taifa likateuwa watendaji wataohusika na utoaji wa mikopo wakiwa chini ya kitengo kilichojulikana kama bodi ya mikopo ya elimu ya juu.lakini pindi kikundi hiki kilipoanza kazi kikageuza wanafunzi wanaoomba mkopo kama ni wafungwa na wao ni chombo cha kuwakomesha na kuwashikisha adabu kwa kuwachelewesha na kuwanyima mikopo maskini na kuwapa matajiri na ata wafanyabiashara wasio wanachuo mikopo na kuwatesa ipasavyo wananchi wa ngazi ya chini kwani kama bodi hii inatambua mwanachuo anatoka katika familia maskini iweje ikapita hadi miezi minne toka chuo kifunguliwe bila ya kumpatia fedha ya chakula je mtu huyu anaweza kuishi vip? na pia je inawezekanaje kwa mwanachuo kuenda katika mafunzo yake ya vitendo bila ya kumpatia pesa na badala yake watumishi hawa wanaziweka pesa zake kwenye mabenki ili wale riba, si hivyo tu bali ukisoma katika tarifa yao utaona wanawapa fedha kidogo za nauli kuliko wanazoandika na kujinufaisha,ona vijana wadogo wa taasisi hii wanaolipwa mishahara midogo kadri ya laki nne wanvyojenga maghorofa mbezi beach na masaki je huu ndio mshahara wao unavyotumika hau ni wapi wanapata pesa hizi? je kumuandikia mtu pesa nyingi za nauli na kumpa kidogo sio ufisadi? je taifa linatambua ya kuwa watu waliopewa dhamana ya kuwaudumia wasomi wanawageuza watumwa na wafungwa, napenda kutoa wito wangu kwa mfano mtu anayepewa jukumu hili kwanza awe ni mzalendo, awe na uzoefu kwani hapa si mahali pa kujifunza kazi kwenye elimu ya juu, na nashindwa kutambua ya kuwa je bodi hii inachombo chochote kinachoisimamia kwani kina uhuru mkubwa amboo unauzidi hata wa mahakama, napenda kuwafahamisha ya kuwa mimi sisemi kwa kubahatisha kwani hata leo hii wapo wanachuo wa mzumbe wlioanza mafunzo kwa vitenda oktoba 12 mpaka leo ni zaidi ya mwezi lakini pesa zao zimekaliwa na watumishi hawa wakizizalishia hili wapate riba ndio waje kuwapa je watu hawa wanajua jinsi wanachuo awa wanavyoteseka au ni namna ya mfumo wao wa kuwaadabisha kama wafungwa wao wa kielimu? mbaya zaidi wazazi na wananchi katika taifa hili kuwa kimya kwa jambo hili huu ni upuuzi kutuletea kilimo kwanza huku ukiwaacha watu wakiua elimu ya juu, hakuna taifa litaloendelea kwa kutesa wasomi wake,na kama ikitokea sisi ndio tutakuwa wakwanza kwani tumebaki kuwa tifa linalojivunia kwa kujigamba kuwa sii ndio taifa la kwanza kwa kubuni mambo, wako wapi usalama wa taifa kwani hawaoni wenzao CIA wanvyolinda maslahi ya marekani kwani ingewapasa hata kuua watu wachache hili taifa liendelee, au na usalama wa tifa wanahitaji mwekezaji? au menejimenti mpya, nisingependa kuongelea PCCB WALA POLISIkwani kila mtu anajua utendaji wao, naomba taifa lifikie mahali liwashitaki na kuwapandisha kizimbani watumishi wa bodi hii na ikibidi wafilisiwe mahekalu yao

Napenda kuwaeleza ya kuwa hipo siku watawajibika kwa wanayoyafanya sasa hata wakiwa kaburini tutafunga pingu juu ya makaburi yao ili umma utambue ujuma yao,

napenda kuwajulisha elimu ni bahari na wasizani kuna namna ya kuhuma watazozificha daima

MUNGU IBARIKI TANZANIA

MUNGU WABARIKI WANACHUO

MUNGU WALAANI WATUMISHI WA BODIGODWIN CHACHA

MZUMBE UNIVERSITY

0718122081

No comments:

Post a Comment