Wednesday 30 December 2009

KIKWETE ANGOJEA HISANI YA MAKADA

Wakati miezi takribani tisa imebaki kabla ya uchaguzi mkuu,jahazi la mkuu wa nchi inaonekana kupoteza nguvu katika chama na hata makundi ya kijammii.

Kikwete anakabiliwa na upinzani mkubwa sana, unaohatarisha nafasi yake kushinda kuwa mgombea wa chama chake, hii inatokana na mahusiano yanayojengwa na katibu mkuu Makamba, kutothamini mawazo ya wakongwe kama akina joseph Warioba ,Dk salim Ahmed salimu,

kitendo kinachoendelea kujenga makundi,ambayo inadhaniwa uwenda yakamuunga mkono,FREDRIC SUMAYE pindi atapotangaza azma yake ya kugombea urais.

Makada mashuhuri wamesikika wakisema, chama hakiwezi kuendeshwa kwa vitisho na matusi, bali hoja na kufuata misingi na hitikadi ya chama.
Imefika wakati viongozi wa chama wanadhubutu kuwahita wanachama wengine wehu, watu walioshika nyadhifa mbalimbali. na bado wengine wakiwa wanamajukumu mbalimbali ya kichama.

Kwa upande wa wananchi wa kawaida wanakiona kitendo cha rais kuwa kimya huku rasilimali za taifa zikiibiwa kwa kisingizio cha mikataba ya kimataifa ni uzembe unaoligharimu taifa.

Tazama misamaha ya kodi pamoja wanayopewa wageni katika nchi yetu ni mikubwa kuliko katika nchi yeyote.
Cha kusikitisha ni unaposikia waziri anasema makampuni hayajarudisha mitaji waliowekeza.

Huu ni ukosefu wa mtazamo ,kusubiri wawekezaji wapate faida, kwani mbona mwananchi wa kawaida anapowekeza katika biashara mfano daladala, anaanza kulipa kodi moja kwa moja na hangoji mpaka kurudisha mtaji wake.

Kutokana na mapungufu yaliyojitokeza katika utawala wa awamu ya nne. Ambayo yameiingiza nchi katika udini, ukabila na kambi za kisiasa.

Imesababisha kujiwekea watika mgumu wa kurudi kipindi kingine kwani nani ambaye hafahamu nguvu za kambi ya mwandosya ,ya akina salim ahmed salimu na fredric sumaye pindi zitapojiunga.

je kikwete anaweza kukabiliana nazo au atamtumia makamba kujibu hoja kwa matusi.

Ni vema rais kikwete, akaonyesha mfano bora katika taifa letu, kwa kutogombea tena, kwani atakuwa amejijengea heshima kubwa ya kutong"ang"ania madaraka.

kwa kadri ninavyomfahamu kikwete hashindwi kutogombea tena, lakini shinikizo kubwa linatoka katika wafuasi wake ambao walichangia kampeni kwani wengi wao hawajachota faida za kutosha.

Bila ya mabadiliko CCM inaifuata historia KANU na ZANU PF,kwani nani aliyeota ndoto kwamba KANU kitatoweka katika siasa za Kenya , au ZANU PF katika siasa za Zimbabwe?

Serikali ya CCM imepoteza vipaombele, imebaki kucheza ngoma ya maisha bora kwa kila mtanzania, ari mpya kasi mpya na kilimo kwanza .

Cha msingi cha kujiuliza ni nini kitatufanya kuendelea kumuunga mkono rais wa kambi mojawapo ya CCM, kwani wote tunafahamu CCM ilitokana na muungano wa TANU na ASP lakini kadri siku zilivyoenda nguvu ya CCM ikatawaliwa na waliokuwa wanachama wa TANU.

Lakini mgogoro wa sasa hautokani na wanachama wa ASP na TANU. si mvutano kati ya wazanzibar na wabara ndani ya chama kwani wazanzibari walishasalimu amri na kuachia nguvu za chama ndani ya wabara.

Mgogoro wa sasa unatokana na watawala wa sasa kutotaka kusikiliza ushauri wowote toka kwa kambi zilizoshindwa 2005, hivyo basi kuzifanya kambi hizo kama vikundi vya wahaini.

Kwa upande wetu wananchi tunafurahi kwani makundi ndani ya CCM yamefanya tufahamu mengi kuhusu madhara gani ya kununua madaraka.kambi ndani ya vyama zinamadhara gani?

Kugawanyika ndani ya CCM ni funzo kubwa kwa vyama chipukizi kama UDP, NCCR
CHADEMA n.k kwamba lazima waunde umoja na kutoa elimu kwa wanachama ya ni jinsi gani ya kuendesha siasa ndani na nje ya chama.

Mwalimu NYERERE hakukosea kuanzisha chuo cha mafunzo kivukoni,kwani kilichangia kuimarisha siasa za chama ndani na nje na kujenga mifumo ya uongozi katika sekta ya siasa.

lazima wanachama kama Makamba na Tambwe hiza muhamiaji toka CUF watambue kejeli si sera za chama kwani zinaongeza mgawanyiko.

Siasa na unajimu ni vitu tofauti huwezi ukaongoza nchi kwa kufuata wapigaramli na wanajimu kwani yuko wapi Mobutu seseseko na kundi lake la wapunga pepo, wapunga pepo walimtabilia kwamba angeshinda vita zidi ya Banyamulenge matokeo yake ni kushindwa kwa kishindo.

Tamko la ikulu kuhusu wapigaramli limetushitua kidogo kuhusu je ikulu imeamua kuanza siasa za maruani au kwa nini watoe ufafanuzi kuhusu tamko hilo, kuna mawazo mangapi yamepingwa au kutotolewa ufafanuzi.

Kushindwa kwa siasa za sera,kunapelekea kubadilika kwa siasa toka wito kuwa uhadui na kuhatarisha amani na mshikamano wa nchi yetu.

Kikubwa tunachokiona ni kukoma kwa sera zilizopo. Ni lazima zibuniwe zitazoendana na wakati, kwani tatizo si kwenye vyama vya siasa tu bali ata katiba nayo ni tatizo ukisoma katiba kuna vifungu vinavyopingana na vingine vikikandamiza jamii fulani.

mgawanyiko ndani ya CCM umemuweka rais katika wakati mgumu na ikisadikika ndio unaochangia kuzorota kwa afya yake na kusababisha kuanguka mara kwa mara.

nakama hii ndio sababu ya kuanguka kwake, sisi wapitanjia tunapatwa na hofu kubwa. kama afya ya kiongozi mkubwa wa nchi yetu, kwani si lazima uwe daktari ili utambue kwamba wagonjwa wanamahamuzi gani? je nchi yetu inamfumo gani wa kuzuia mahamuzi mabaya yanayoweza kutolewa na rais wa jamhuri ya Tanzania.

Mgongano ndani ya CCM unasababisha jamii itambue siasa zina faida kiasi gani na malengo ya wanasiasa ni yapi? kwani kama siasa isingekuwa na faida vikumbo kati ya wagombea ubunge na urais vingetoka wapi? na siasa chafu ndizo zimepelekea kumweka rais katika wakati mgumu , ata kupelekea kuiweka hatma ya rais mikonomi na hisani ya makada wa chama hicho.

hii ni hatari kubwa kwani inaweza kupelekea rais kufikiria kutumia madaraka yake ndani ya serikali kuzima uhasi ndani ya chama chake.

Taifa na vyama vya siasa lazima viangalie maslai ya taifa kwa kuboresha mifumo yake ya kiutendaji kwa mfano haikuwa sahihi kwa makamba kutumia kauli ya chama kwamba kitamuunga mkono 2010 bali alitakiwa aseme yeye kama yeye atakuwa katika kambi ya Kikwete kwani wanachama wote wanahaki ya kuomba nafasi stahili ndani ya chama chao.

Mbona wabunge waliotawala kipindi kimoja wanajitokeza wapya kuwapinga? au Cheo cha katibu mkuu wa Chama ni cha usemaji wa rais.

Makamba ana mengi ya kujifunza lakini hili la matusi na kejeli limesababisha kidonda kikubwa ndani ya chama chake na ata mustakabali wa rais.

Natoa wito kwa wanachama wa CCM wataojitokeza kupingana na rais 2010 wajitokeze si tu kwasababu wana chuki na rais bali wana uwezo wa kuongoza taifa la Tanzania na ni haki yao ya msingi.

siasa ndani ya CCM lazima iwe kwa misingi ya sera na si makundi na chuki, kwani kuendeleza chuki kutapelekea uhasama na kudunisha maendeleo ya jamii ya Tanzania.

Ushauri wangu kwa kikwete kama anaona nayeye pia anaweza kuongoza kipindi cha pili agombee kwa hiari yake na si kushinikizwa na wapambe kwani kila mtu atapima kina cha maji kabla ya kujitosa.

Mungu ibariki tanzania
Godwin chacha 0718122081
www.godwinchacha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment